Hutekeleza ahadi zao wanapoahidiana na wanaadamu wenziwao maadamu ni katika mipaka ya Allah (s.w).
Ahadi kubwa wanayotoa Waislamu mbele ya Allah (s.w) ni shahada; pale wanapo ahidi kuwa hawatamshirikisha Allah (s.w) na chochote na kwamba wataishi maisha yao yote kwa kufuata mwongozo wa Allah (s.w) kupitia kwa Mtume wake, Muhammad (s.a.w). Rejea (6: 162 -163)Katika Suratul-Fur-qaan sifa za Waumini zinabainishwa tena kama ifuatavyo:
“Na waja wa Rahmaan; Ni wale wanaokwenda ulimwenguni kwa unyenyekevu; na wajinga wakisema nao (maneno mabaya) huwajibu (maneno ya) salama. (25:63).
Na wale wanaopitisha baadhi ya saa za usiku kwa ajili ya Mola wao kwa kusujudu na kusimama. Na wale wanaosema:“Mola wetu! Tuondolee adhabu ya Jahannam, bila shaka adhabu yake ni yenye kuendelea(25 :64-65).
Hakika hiyo (Jahannamu) ni kituo kibaya na mahali (pabaya kabisa) pa kukaa ”.Na wale ambao wanapotumia hawatumii kwa fujo wala hawafanyi ubakhili, bali wanakuwa katikati baina ya hayo. (25:66-6 7)
Na wale wasiomuomba mungu mwingine pamoja na Allah, wala hawaui nafsi aliyoiharamisha Allah ila kwa haki, wala hawazini; na atakayefanya hayo atapata madhara (papa hapa ulimwenguni).(25:68).
Na atazidishiwa adhabu siku ya Kiyama na atakaa humo kwa kufedheheka milele (25:69).
Ila yule atakayetubia na kuamini na kufanya vitendo vizuri, basi hao ndio Mwenyezi Mungu atawabadilishia maovu yao kuwa mema; na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe, Mwingi wa ku reh em u. (25:70).
Na aliyetubia na kufanya wema, basi kwa hakika yeye anatubu kw eli kw eli kw a Mwenyezi Mungu.(25:71)
Na wale ambao hawashuhudii shahada za uwongo, na wanapopita penye upuuzi, hupita kwa hishima (yao). (25:72)
Na wale ambao wanapokumbushwa aya za Mola wao haw aziangukii kw a uziw i na upofu.(25:73)
Na wale wanaosema: “Mola wetu! Tupe katika wake zetu na wototo wetu yaburudishayo macho (yetu) (nyoyo zetu), na Utujaalie kuwa waongozi kwa wamchao (Mungu). (25:74).
Hao ndio watakaolipwa ghorofa (za Peponi) kwa kuwa walisubiri, na watakuta humo hishima na am ani(25 :75).
Wakae humo milele; kituo kizuri na mahali pazuri (kabisa pa kukaa.) (25:76)
Kutokana na aya hizi tunajifunza kuwa sifa za Waumini ambao hapa wameitwa “Waja wa Rahman” ni pamoja na: