Waumini wa kweli waliofuzu huchunga amana. Hutunza amana aliyopewa na kuirejesha au kuitumia kwa mujibu wa maelekezo ya mwenyewe.
Amana kuu aliyopewa mwanaadamu na Mola wake ni kule kufadhilishwa kwake kuliko viumbe vingine vyote ili asimamishe Ukhalifa (utawala wa Allah) katika ardhi kama tunavyokumbu shwa katika Qur-an:
“Kwa yakini Sisi Tulidhihirisha amana kwa mbingu, ardhi na milima,vikakataa kuichukua na vikaiogopa,lakini mwanaadamu aliichukua. Bila shaka yeye ni dhalimu mkubwa, mjinga sana ”. (33:72)