(vii)Hufanya bias hara na Allah (s.w)

(vii)Hufanya biashara na Allah (s.w)


Wanafanya jitihada za makusudi kwa kutumia mali zao na kujitoa muhanga nafsi zao ili kuhakikisha kuwa dini ya Allah inasimama katika jamii.


Yaani wanajitahidi kwa jitihada zao zote ili kuzifanya sharia za Allah (s.w) ziwe ndizo zinazotawala harakati zote za maisha ya jamii.


Pia sifa za Waumini zinabainishwa katika Suratul-Muuminuun kama aya zifuatavyo:Hakika wamefuzu Waumini ambao katika swala zao huwa wanyenyekevu.(23:1-2)Na ambao hujiepusha na Lagh-wi (mambo ya upuuzi).


Na ambao Zaka wanaitekeleza.(23:3-4)Na ambao tupu zao wanazihifadhi isipokuwa kwa wake zao au kwa (wanawake) wale iliyomiliki mikono yao ya kuume. Basi hao ndio wasiolaumiwa.(23:5-6)Lakini anayetaka kinyume cha haya, basi hao ndio warukao mipaka.


Na ambao amana zao na ahadi zao w anaziangalia (23:7-8).Na ambao swala zao wanazihifadhi. Hao ndio w a rith i(2 3:9-10).Ambao watarithi Firdaus (Pepo ya daraja ya juu) wakae humo milele. (23:11)
Kutokana na aya hizi tunajifunza kuwa waumini wa kweli waliofuzu na watakaostahiki kupata pepo ya Firdaus, ya daraja ya juu kabisa ni wale wanaojipamba na sifa zifuatazo: